avatar
Your name :

or login

Add Song
New comments

Dizasta Vina - Chupa moja ya ziada

 
0
Copied!
Kalala chini ubongo na fuvu vimetengana
Hatoi sauti hana hata nguvu ya kulalama
Macho yetu yanagongana ya kwangu yanaona haya
Natamani kufumba maana naona uchungu kumtazama

Ni butwaa siwezi eleza hali yake
Mifupa imezagaa kadhaa haipo mahali pake
Waungwana wamejaa wanauliza ka' mi' timamu
Damu nyingi nataka niamini ni filamu

Hata nikifumba macho naona jambo hili hili
Nafsi yangu inahofu na inatukana kwa siri siri
Ameumia siwezi kumtazama mara mbili mbili
Mguu mmoja umetengana na kiwiliwili

Kweli nimeamini utu wa mtu ni uhai wake
Mja amelala watu wamewahi karai lake
Wengi wanatabiri tanzia bila kuficha
Wema wanalia na mabazazi wanapiga picha

Amechanika nyama kuonyesha nyama si tunu
Anapata maumivu kabla hajaikumbata huru
Anaonyesha kuwa mwili ni kasha lisilodumu
Na kujua siku ya uhai kutoka ilivyo sumu

Mtoto wake analia ameisoma ajenda
Kuwa baba uhai umetoka na roho yake ishakwenda
Anahitaji uthibitisho na picha inajieleza
Ananiona mimi nami sina ninachokiweza
Natamani niamke nigundue picha nicheke
Au labda naota ndoto ya kutisha nikeshe
Huku wapita njia wakipiga kelele
Kuona mtoto anakuwa yatima milele

Chupa moja ya ziada
Chupa moja ya ziada

Nilipigiwa simu ikisema njoo baa
Maana mtungi wa nyumbani haunogi
Nikalewa kisha nikataka kuondoka
Mpumbavu mwingine akasema one for the .....

Chupa nikazipanga panga
Mfuko ulipokauka wakanijaza
Nikanywa nikijitapa kama mjanja
Wana wakipiga kelele kuniita
(mwamba mwamba)

Sikio la mlevi likashika habari
Sifa walizonipa zikanishika hatari
Sikuwaza kuwajibika kuwa nani nitamuumiza
Nilikuwa mbinafsi kiasi nilishindwa kujali

Labda ningebakia kwenye kijiwe nongwa cha Biafra
Ninywe kahawa nikisikiliza soga za siasa
Ningekunywa kidogo labda nisingerudia
Nimeua mpita njia sababu ya chupa moja tu ya ziada
Nimefanya kosa na muda unakwenda hasa
Hasa nitaongea kipi? kipi nitaeleza sasa?
Sababu chupa moja tu ya ziada
Mke anamkosa mume aliyempenda
Mtoto anampoteza baba

Maji yameshamwagika nani wa kunifundisha lugha?
Niseme kwa nani ama nani wa kuunganisha nyufa?
Nani wa kuujuza umma kuwa nami najuta nafsi?
Nani asimamishe siku kisha akaurudisha muda?

Malipo gani yakurudisha pumzi kwenye mwili
Uamke tena? uhai hata kwa hela tu haukopwi
Adhabu gani itamfaa mpuuzi kama mimi
Asiyejua maana ya pumzi?
Maana hata jela tu hainitoshi

Hata nikiamua kufunga na kuuungama
Siwezi kuzuia uuma wa watu wakiungana
Kuamua kumwaga damu kwa mja nilie na laana
Nife nilipe deni kwa hii dhuluma niliyoifanya

Muda umesimama moyo unaingia baridi
Nimemgonga na gari picha inanijia saa hizi
Mja anakata roho picha inayoingia zaidi
Ni kuona vibaka wanaiibia maiti
Chupa moja ya ziada
Ziada ziada ziada ziada ziada
Chupa moja ya ziada

SoundCloud:

edit soundcloud

YouTube:


More Dizasta Vina lyrics

Dizasta Vina

No Foto

Song Description

Biography

New Lyrics

Various Artists - Under a Glass Moon | Lyrics
{Instrumental Intro} {Intro} Tell me, remind me Chase the
Samuel Vincent - Royal Fool | Lyrics
{Verse} Every time you walk in the room you appear funny Dancing in the streets
YANFI 21 - ESCALATOR | Текст песни
{Интро} M-M-Muffin on the track {Припев} Я
Emocionado - CHADY | Lyrics
{Verse} Look what you do to me And I lost myself in your smile I even
Clay Hollis - Floatin' Down The River | Lyrics
{Verse 1: Clay Hollis} You know a girl can't be too careful Don't
​wewantwraiths - Dopamine | Lyrics
I got no more left to say, I mix codeine with the pain Every day is not the same, without my
Cheerleader Roadkill - Sick of Playing | Lyrics
{Verse 1} Can't really talk right now I'm way too busy Fucking
V311ax - Я так хочу | Текст песни
{Интро} Я так хочу, я так хочу, я так хочу Я так хочу, я так хочу, я так
Ensade - Сожгла машину | Текст песни
{Текст песни «Сожгла машину»} {Интро} В мыслях я давно сожгла